Mfalme wa masauti (king of the best melody) Christian Bella amelazwa hospitalini nchini Congo juzi, Bella aliugua ghafla. Christian Bella alikuwepo nchini Congo pamoja na TID,takribani wiki mbili kwaajiri ya show, ambapo tayari ameshafanya show kadhaa nchini humo. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Bella ametupia picha akiwa amelazwa hospitalini huku akiwa ametundikiwa dripu la maji ambapo inaonekana hali yake sio nzuri.