Mkali wa muziki wa R&B nchini Tanzania Diamond, leo amezindua rasmi bidhaa yake mpya ukiachana na ile ya kwanza ya "perfume", leo amekuja na nyingine inayoitwa "Diamond Karanga" .Diamond amesema " Bidhaa hiyo itakuwa inapatikana nchi nzima na Afrika mashariki kwa ujumla, kwa bei nafuu kabisa kwa shiling miatatu tu "300/=" bei ya rejereja kwa pakiti moja na shilingi elfu 20,000 /= kwa boksi moja lenye pakiti mia moja (100) ndani ambayo ukiuza unapata faida ya elfu kumi".