Jerry Moro Aachiwa Huru Leo Baada Ya Kumaliza Kifungo Chake

Msemaji wa Yanga Jerry Muro leo amemaliza kifungo chake cha mwaka mmoja kwa kutojihusisha na masuala ya soka, anatoka na kuwaacha waliomuhukumu wapo gerezani. Mnamo tarehe 2/07/2016 msemaji wa timu ya Yanga Jerry Muro alifungiwa na TFF kutojihusisha na masuala ya soka kwa mwaka mmoja na kulipa faini ya shiling milion 3.Jerry Mjuro alifungiwa kutokana na kutumia lugha za uchochezi katika matangazo ya televisheni kabla ya mechi kati ya Yanga na TP Mazembe.