Picha Kali Alizopiga Rihanna Wiki Hii
5:45 AM
Huu ndiyo muonekano mpya wa Rihanna ndani ya wiki hii, Watu wengi wamezoea kumuona Rihanna akiwa amevaa mitindo fulani hivi, lakini wiki hii ameamua kuja tofauti kidogo kama tulivyo mzoea, Hizi ndizo picha alizopiga wiki hii.CLICK HERE
Video: Barnaba Ameamua Kuja Na Haya - TUNAFANANA
2:55 AM
Jerry Moro Aachiwa Huru Leo Baada Ya Kumaliza Kifungo Chake
11:09 AM
Msemaji wa Yanga Jerry Muro leo amemaliza kifungo chake cha mwaka mmoja kwa kutojihusisha na masuala ya soka, anatoka na kuwaacha waliomuhukumu wapo gerezani. Mnamo tarehe 2/07/2016 msemaji wa timu ya Yanga Jerry Muro alifungiwa na TFF kutojihusisha na masuala ya soka kwa mwaka mmoja na kulipa faini ya shiling milion 3.Jerry Mjuro alifungiwa kutokana na kutumia lugha za uchochezi katika matangazo ya televisheni kabla ya mechi kati ya Yanga na TP Mazembe.
Picha Kali Nne (4) Alizopiga Zari (Zari the Boss lady) Zinazo Zungumziwa Zaidi Kwenye Mitandao Leo Ya Kijamii.
5:26 AM
Hizi ndizo picha kali tano za leo alizopiga Zari ambazo zimekuwa zikienea kwenye mitandao ya kijamii alizopiga akiwa na mwenza. Zari Hassan, maarufu kama (Zari the boss lady) ni mke wa Diamond,Zari ni mwanamke anayejishughulisha na muziki, mwanamitindo na ujasiliamali ambapo shughuli zake anazifanyia Afrika ya Kusini.Kupitia ukurasa wake wa Instagram leo Zari ametupia picha tano alizo piga akiwa na mume wake ambaye ni Diamond Platnumz,picha hizo ambazo zikiwa na tafsili ya upendo uliyoshamili kati yao hao wawili.
Triplets Ghetto Kids Wapata Shavu Kutoka Kwa Wasanii Wa Marekani, Kwenye BET Awards 2017
10:21 AM
Wasanii wa muziki kutoka nchini Uganda wanojulika kama "Triplets Ghetto Kids" wamekutana na wasanii wakubwa kutoka nchini Marekani ambao waliudhuria show yako walioifanya na French Montana wimbo "Unforgettablle". Wasanii hao wa Marekani ni ambao walikutana nao na kupiga picha ni DJ Khaled, Fat Joe na rapper Chance.
Ghetto Kids ambao wameweza kuitangaza Afrika baada ya Performance ya BET (Blank Entertainment) ya June mwaka 2017 huko Marekani .Watoto hao wamewafurahisha na kuwavutia sana wamerekani na kuacha historia kubwa nchini humo. KUTAZAMA VIDEO YAO BOFYA HAPA...
Diamond Azindua Bidhaa Zake Mpya Leo, Hizi Hapa
10:10 AM
Mkali wa muziki wa R&B nchini Tanzania Diamond, leo amezindua rasmi bidhaa yake mpya ukiachana na ile ya kwanza ya "perfume", leo amekuja na nyingine inayoitwa "Diamond Karanga" .Diamond amesema " Bidhaa hiyo itakuwa inapatikana nchi nzima na Afrika mashariki kwa ujumla, kwa bei nafuu kabisa kwa shiling miatatu tu "300/=" bei ya rejereja kwa pakiti moja na shilingi elfu 20,000 /= kwa boksi moja lenye pakiti mia moja (100) ndani ambayo ukiuza unapata faida ya elfu kumi".
Wananchi Leo Maeneo Mbalimbali Nchini Walivyo Jitokeza Kufuatilia Ripoti Ya Mchanga Wa Madini
7:59 AM
Kufuati ripoti ya pili ya mchanga wa madini ambayo ilikuwa inawasilishwa leo kwa raisi Ikulu jiji Dar es Salaam kuanzia mida ya saa tatu asubuhi, wananchi sehemu mbalimbali nchini walijitokeza kufuatilia tukio hilo kupitia runinga (Television, Tv).
Kupitia ripoti hiyo ya pili iliyowasilishwa rais Dr. Magufuli , Rais Dr. John Magufuli amesema kuwa "Serikali idai fedha kwenye kampuni ya Acacia ambayo imekua ikiliibia taifa, Nasema hakuna mchanga kutoka nje. Naomba sheria ya Gesi ipitiwe upya ili tuwe na sheria nzuri, wanasheria wako kibao lakini mikataba ndo hii, wamesoma nini?".
"Wahusika wote waliotajwa kwenye ripoti hii vyombo vya dola viwahoji na kubaini ukweli juu ya jambo hili" amesema rais Dr. Magufuli leo.
Majina Ya Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga Na Kidato Cha Tano Na Vyuo Vya Ufundi 2017, Haya hapa
1:22 PM
Haya ndiyo majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujinga na kidato cha tano na vyuo vya ufundi.
Ziara Ya Jokate Mkoani Ruvuma-Songea Awakusanya Watu
1:22 PM
Jokate Mwegelo afanya ziara katika mji wa Songea taklibani wiki moja , akiwa Songea Jokate ameweza kutembelea maeneo mbalimbali kuwasalimu ndugu na jamaa, Picha joketi akiwa na waanafunzi wa sekondari alipotembelea mashindano ya umiseta walikoweka kambi katika chuo cha ualimu Matogoro mjini Songea.
Picha Jokate akiwa ametembelea kituo cha redio cha keyfmz 90.5 mjini Songea .
Christian Bella Abanwa Akiwa Huko Nchini Congo
1:02 PM
Mfalme wa masauti (king of the best melody) Christian Bella amelazwa hospitalini nchini Congo juzi, Bella aliugua ghafla. Christian Bella alikuwepo nchini Congo pamoja na TID,takribani wiki mbili kwaajiri ya show, ambapo tayari ameshafanya show kadhaa nchini humo. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Bella ametupia picha akiwa amelazwa hospitalini huku akiwa ametundikiwa dripu la maji ambapo inaonekana hali yake sio nzuri.
Jinsi Ya Kupangilia Vitu Ndani Ya Nyumba
3:08 AM
Ili nyumba iweze kupendeza ni lazima ujue kupangilia vitu vyako ndani kama kwenye picha hapo juu na chini.Watu wengi huwa wanashindwa jinsi ya kupangilia vitu katika nyumba mfano kuweka pazia au sofa ambazo zinaendana na kuta za nyumba. Ili nyumba iweze kupendeza ni lazima kuta za nyumba ziendane na pazia au sofa.